
Baada ya ubalozi wa Marekani mjini Baghdad nchini Iraq kulengwa kwa shambulio, vyanzo vya habari vimeripoti kuharibiwa kwa mfumo wa ulinzi wa anga wa ubalozi huo.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Associated Press maafisa wa usalama wamethibitisha kwamba kombora moja lilipiga eneo la kutua helikopta ndani ya ubalozi wa Marekani.
Katika muktadha huo, chanzo kimoja cha usalama cha Iraq kiliiambia Al Jazeera kwamba mfumo wa ulinzi wa anga wa ubalozi huo pia ulikuwa miongoni mwa malengo ya shambulio hilo.
Aidha, imeripotiwa kwamba rada iliyokuwa imewekwa katika ubalozi huo imeharibiwa
Kufuatia kuharibiwa kwa mfumo wa ulinzi wa ubalozi wa Marekani, vikosi vya usalama vya Iraq vilifunga njia zote za kuingia na kutoka katika Ukanda wa Kijani (Green Zone) wa Baghdad.
Ukanda huo wa Kijani unahifadhi ubalozi wa utawala vamizi wa Marekani.
Hayo yanajiri siku moja baada ya Makao Makuu ya Kamandi ya Kati ya Marekani (CENTCOM) kuetangaza ‘kuanguka’ kwa ndege yao ya kijeshi ya kujaza mafuta angani katika eneo la magharibi mwa Iraq, na kutaja tukio hilo kuwa eti ni “ajali”. Hatahivyo Harakati ya Muqawama au Mapambano ya Kiislamu nchini Iraq imetangaza rasmi kutungua ndege hiyo ya jeshi la kigaidi la Marekani.
Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa habari hiyo, kinyume na madai ya Jeshi la Marekani, mwandishi wa habari wa mtandao wa CBS wa Marekani aliripoti kuwa ndege hiyo ya kujaza mafuta ilitunguliwa kwa kombora kuanguka. Kwa mujibu wa taarifa yake, ndege nyingine ya kujaza mafuta pia ilipigwa, lakini iliweza kufanikiwa kutua ‘Israel’.
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Iraq imetangaza kupitia taarifa rasmi kuwa imeidungua ndege hiyo ya kujaza mafuta ya Marekani wakati ikiwa agani katika eneo la magharibi mwa Iraq.
Harakati hiyo imesema wapiganaji wake, wakitetea mamlaka na anga ya taifa lao, waliidungua ndege hiyo katika eneo la magharibi mwa Iraq kwa kutumia kombora.
Harakati za Muqawama nchini Iraq zimekuwa zikilenga jeshi la kigaidi la Marekani nchini humo kulipiza kisasi vita vinavyoendelezwa na Marekani kwa kushirikiana na utawala haramu wa Israel dhidi ya Iran.