Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha na Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Cecilia Daniel Paresso, ametoa mchango wa mbao zenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki tano (2,500,000/=) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Karatu.

Mbao hizo zimekabidhiwa rasmi Leo mbele ya viongozi mbalimbali na wanachama wa CCM wilaya, ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa awali katika kuunga mkono juhudi za chama za kuboresha mazingira ya kazi na makazi ya watumishi wake.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mheshimiwa Paresso alisisitiza umuhimu wa mshikamano na ushirikiano katika kujenga na kuimarisha miundombinu itakayowawezesha watumishi wa chama kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Viongozi wa CCM Wilaya ya Karatu walimshukuru Mbunge huyo kwa mchango wake, wakieleza kuwa msaada huo utakuwa chachu muhimu ya kuharakisha ujenzi wa nyumba hizo na kuwahamasisha wadau wengine kujitokeza kuchangia mradi huo.Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha na Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Cecilia Daniel Paresso, ametoa mchango wa mbao zenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki tano (2,500,000/=) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Karatu.

Mbao hizo zimekabidhiwa rasmi Leo mbele ya viongozi mbalimbali na wanachama wa CCM wilaya, ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa awali katika kuunga mkono juhudi za chama za kuboresha mazingira ya kazi na makazi ya watumishi wake.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mheshimiwa Paresso alisisitiza umuhimu wa mshikamano na ushirikiano katika kujenga na kuimarisha miundombinu itakayowawezesha watumishi wa chama kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Viongozi wa CCM Wilaya ya Karatu walimshukuru Mbunge huyo kwa mchango wake, wakieleza kuwa msaada huo utakuwa chachu muhimu ya kuharakisha ujenzi wa nyumba hizo na kuwahamasisha wadau wengine kujitokeza kuchangia mradi huo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *