Katika siku ya 17 ya vita vya Mashariki ya Kati, jeshi la Israel limetangaza leo Jumatatu, Machi 16, kwamba limeanzisha “operesheni ndogo ya ardhini” dhidi ya kundi la wanamgambo wa Kishia la Hezbollah linalounga mkono Iran kusini mwa Lebanon. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Katika siku za hivi karibuni, wanajeshi wa Israel kutoka Kitengo cha 91 wameanza operesheni ndogoza ardhini dhidi ya ngome muhimu za Hezbollah kusini mwa Lebanon, zenye lengo la kuimarisha eneo la ulinzi wa mbele” katika eneo la Lebanon, kando ya mpaka kati ya Israel na Lebanon, jeshi limesema katika taarifa.

Kulingana na Wizara ya Afya ya Lebanon, mashambulizi ya Israel nchini humo tangu Februari 28 yameua watu wasiopungua 850, wakiwemo wanawake 66, watoto 107, na wafanyakazi wa afya 32. Pia kuna watu 2,105 waliojeruhiwa na zaidi ya 800,000 waliokimbia makazi yao.

Kwa upande mwingine nchi za Ghuba zinaendelea kulengwa na ndege zisizo na rubani, haswa Riyadh, ambayo imetangaza kuwa imenasa zaidi ya ndege zisizo na rubani 60 katika eneo lake tangu usiku wa manane Jumatatu, Machi 16, kulingana na Wizara ya Ulinzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *