#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limewakamata watu wawili kwa tuhuma za matukio hatarishi yanayohusisha bastola na kupiga risasi hovyo, yanayohatarisha usalama wa jamii.

Kesi ya kwanza imehusisha Ibrahimu Ideva Yusuph (45), mkazi wa Tumbaku, ambaye anadaiwa kumtishia mhudumu wa klabu ya pombe kwa kutumia bastola, akitaka apewe pombe bure.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika eneo la Nanenane, Manispaa ya Morogoro akiwa na bastola aina ya Browning namba B.395661 yenye risasi tano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema silaha hiyo imechukuliwa na Polisi kabla haijasababisha madhara na hatua za kisheria zinaendelea.

Tukio la pili limemhusisha Kishiwa Stanslaus Zumbi (51), mkazi wa Kihonda, Manispaa ya Morogoro, ambaye alikamatwa kwa tuhuma za kufyetua hovyo risasi akiwa katika umati mkubwa wa watu kwenye starehe isivyo halali.

Mtuhumiwa alikamatwa na silaha hiyo ya pistol aina ya Macrov namba AK 0077 na anadaiwa alifyatua risasi nne, jambo lililosababisha taharuki miongoni mwa watu waliokuwa jirani.

Kamanda Mkama alibainisha kuwa tukio hilo lilitokea majira ya usiku na silaha hiyo pia inashikiliwa ili isitumike vibaya tena.

Jeshi la Polisi linawaonya wananchi kuepuka kushughulika na silaha vibaya na kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha usalama wa umma unadumishwa.

Powered by #MCHEZOSUPA:

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *