Mafundisho ya Qur’an katika Mwezi Mtukufu wa Ramadan yameelezwa kuwa yanahimiza amani, upendo na mshikamano katika jamii, jambo ambalo limechangia kuimarisha utulivu na kufanya mazingira kuwa rafiki kwa maisha ya wananchi pamoja na shughuli za biashara.

Akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni ya Mogas Tanzania, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amesema viongozi wa dini wamekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha maadili ya jamii na kusaidia kupunguza vitendo vya uhalifu vilivyokuwa vikiathiri baadhi ya maeneo.

#AzamTVUpdates
✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *