#HABARI: Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Bw. Faris Buruhani, amekutana na waendesha bodaboda na wajasiriamali katika Stendi Kuu ya Biharamulo ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa Operesheni ya “Vijana Daka Fursa na Samia” (VIDAFUSA).

Katika mkutano huo, vijana hao walimueleza kiongozi huyo hitaji lao la kusimamiwa katika maslahi ya kiuchumi na kuhakikisha wanapata fursa stahiki zitakazowawezesha kujikwamua kimaisha.

Bw. Faris ameeleza msimamo wa Serikali kuhusu kiasi cha shilingi bilioni 200 kilichotengwa kwa ajili ya kuwawezesha vijana, huku akisisitiza kuwa ni lazima fedha hizo ziwanufaishe vijana wa Kagera kwa vitendo.

Alibainisha kuwa vijana wanapaswa kutumia sera na mipango ya serikali kuanzisha shughuli halali za uzalishaji na ujasiriamali ili kukuza vipato vyao na kuleta maendeleo katika wilaya hiyo.

Aidha, kiongozi huyo ameeleza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya kuwainua vijana kijamii na kiuchumi nchini kote.

Amewahimiza vijana wa Biharamulo kujipanga na kushirikiana kupitia operesheni ya VIDAFUSA ili kuchangamkia fursa mbalimbali za maendeleo zinazotolewa na serikali, jambo ambalo ni nyenzo muhimu katika kubadilisha maisha yao na mustakabali wa taifa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *