
Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza na waziri wa mambo ya nje David Lammy ameutaja mzozo unaoendelea Ukanda wa Gaza kuwa wa kikatili na usiokubalika kabisa. Lammy alikuwa akihutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, kuhusu kile alichokitaja kuwa janga la Israel na Palestina. Ametetea uamuzi wa nchi hiyo kulitambua taifa la Palestina na kuongeza kwamba watu wake na wale wa Israel wanastahili kilicho bora.
Wakati Israel inazidisha operesheni zake za kijeshi na kuziondoa familia za Wapalestina, hakuwezi kuwa na ufumbuzi wa mgogoro huo isipokuwa hatua za kidiplomasia za pamoja ili kurejesha matumaini ya amani.
Lammy, ambaye pia aliapa kusimama na watu wa Ukraine na Sudan wakati wa migogoro yao inayoendelea, alisema Uingereza itafanya kazi na Marekani na nchi nyingine ili kupata amani ya kudumu.