‎#HABARI: Wakazi wa Kata ya Karema, iliyopo mwambao wa Ziwa Tanganyika mkoani Katavi, wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi, kilimo pamoja na biashara, wameeleza matumaini yao makubwa kufuatia ujenzi wa meli nne za mizigo zitakazokuwa zikifanya safari zake kati ya Bandari ya Karema na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia na Burundi.

‎Wakazi hao wamesema kuwa uwekezaji huo mkubwa katika sekta ya usafiri wa majini unatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu katika ukanda wa Ziwa Tanganyika, jambo ambalo litachochea ukuaji wa biashara za ndani na kuvutia fursa zaidi za uwekezaji katika eneo hilo.

‎Wakizungumza na ITV mara baada ya kushuhudia meli ya nne ikishushwa kwa mara ya kwanza kwenye maji ya Ziwa Tanganyika, wakazi hao wameeleza kuwa hatua hiyo ni ya kihistoria kwa maendeleo ya Karema na maeneo ya jirani.

‎Wamesema pia kuanza kwa safari za meli hizo kutasaidia kupunguza gharama na muda wa usafirishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao ya kilimo, samaki pamoja na bidhaa za biashara ndogo ndogo zinazovuka mipaka ya nchi.

‎Aidha, wakazi hao wamebainisha kuwa mradi huo unatarajiwa kufungua fursa mpya za ajira kwa vijana wa eneo hilo, hususan katika sekta ya usafiri, upakiaji na upakuaji mizigo bandarini, pamoja na huduma nyingine zinazohusiana na shughuli za bandari na usafiri wa majini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *