#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Usambara, mkoani Tanga, Machi 16, 2026 imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtuhumiwa Nassir Masunga (29), dereva na mkazi wa Kange, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kubaka.
Awali imeelezwa Mahakamani kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo dhidi ya Zakia Adamu (20), mfanyabiashara na mkazi wa Kange. Kufuatia tukio hilo jalada lenye namba TAN/IR/1153/2025 lilifunguliwa na baadaye shauri hilo kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya Usambara Tanga kwa namba CC No. 22091/2025.
Akisoma hukumu hiyo, Mheshimiwa Hakimu Mwajombe alisema Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka uliowasilishwa na Wakili Mbilinyi, na hivyo kumtia hatiani mtuhumiwa na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela ili iwe funzo kwa jamii na kusaidia kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania