#HABARI: Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo, Lawrence Mlaki amekabidhi madawati 2000 katika shule 30 za msingi zilizopo katika manispaa hiyo na shule iliyokabidhiwa kwa niaba ya shule zote ni Shule ya Msingi Millenium iliyopo Kata ya Kimara iliyopata madawati 100, hafla hiyo ya ugawaji wa madawati imefanyika Machi 16, 2026.
Akikabidhi madawati hayo Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo, Mlaki amesema kuwa Ubungo inaenda kutatua changamoto ya uhaba wa madawati kwa shule takribani zote zilizopo katika Manispaa hiyo na lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira safi na salama na hii itasaidia katika kupandisha ufaulu wao.
Mlaki amesema, Ubungo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi wapatao laki moja na elfu moja na mpaka sasa kuna jumla ya madawati 24,000 katika shule zote na ili kukamilisha inatakiwa kuwe na madawati takribani 33,000 hivyo changamoto hiyo itatatuliwa haraka kwani awamu ya kwanza imemalizika kwa madawati elfu mbili kutolewa.
“Ni jukumu la Serikali kuhakikisha mazingira salama kwa wanafunzi na sasa Ubungo imebakisha awamu moja ya mgao wa madawati ambao kabla ya bajeti ijayo ya 2027 kuanza changamoto yote itakuwa imeisha kwenye takribani shule zote,” amesema hayo Mlaki.
Sambamba na hilo amewaasa wanafunzi na walimu kuwa wasimamizi wazuri wa madawati hayo kwani Serikali inatoa kwa ajili ya vizazi na vizazi viweze kukalia wanapokuwa mashuleni, hivyo ni wajibu kutunzwa.
Aidha, Mwalimu Mkuu katika Shule ya Millenium Mwl. Failona Kidesu ameshukuru kwa mgao huo ambapo kwa shule hiyo imeondoa changamoto nzima na sasa hakuna darasa ambalo halina madawati.
Nao wanafunzi wa shule hiyo wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa jitihada wanazoendelea kuzionesha kuhakikisha wanakuwa na mazingira salama na bora kwa ajili ya kusoma na kuahidi kuongeza ufaulu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania