Mchambuzi wa Marekani ameeleza kuwa wapiga kura wa nchi hiyo wamekasirishwa na hatua ya rais wa nchi hiyo ya kuiburuta Washington katika vita na Iran.

Wananchi wa Marekani wamekasirishwa na mashambulizi ya kijeshi ya Washington na Tel Aviv dhidi ya Iran katika hali ambayo hivi karibuni Mkuu wa Baraza la Uchumi la White House alitangaza kuwa gharama za vita dhidi ya Iran hadi sasa zinakadiriwa kuwa dola bilioni 12. 

Karen Finney mchambuzi wa Marekani amekiri kuwa kadhia ya vita na Iran imekuwa jambo muhimu miongoni mwa wapiga kura nchini Marekani.

Ameongeza kuwa: Huwenda ikadhaniwa kuwa ajenda kuu ya wapiga kura katika uchaguzi wa katikati ya msimu ni makazi na bima ya afya; lakini ukweli ni kwamba vita ndio suala linaloongoza kati ya yote hayo.

Finney ameeleza kuwa, vijana wamekasirishwa na kuona Trump anakengeuka ahadi yake ya kutoitumbukiza Marekani vitani. Baadhi ya watu hao au baadhi ya jamaa zao ni wanajeshi wa Marekani. Amesema, sasa wazazi wanahofia kutuma watoto wao kupigana katika vita dhidi ya Iran. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *