
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuharakisha ukuaji wa uchumi wa nchi.
Ameeleza kuwa kutokana na kupungua kwa misaada kutoka nje, ni muhimu kuongeza juhudi za ukusanyaji wa kodi ili kusaidia maendeleo ya taifa. Pia amesema Serikali inapanga kurekebisha sheria ya Public Private Partnership (PPP) ili kuboresha ushirikiano na sekta binafsi katika miradi mikubwa.

Aidha, ametoa wito kwa taasisi za serikali, sekta binafsi, wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi kwa ujumla kushirikiana katika ulipaji wa kodi ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo 2050. SOMA: Serikali kupitia mapenddekezo 284 ya kodi