Wanafunzi watatu wafa kwa radi DarWanafunzi watatu wafa kwa radi Dar

DAR ES SALAAM; Wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Msongola wilayani Ilala, Dar es Salaam wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi, huku wengine wawili wakijeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea Machi 18, 2026 majira ya saa 5:00 asubuhi katika eneo la Msongola.

Amesema waliojeruhiwa ni Nadri Maneno (8), mwanafunzi wa darasa la tatu na Mahadi Ramadhan (8), mwanafunzi wa darasa la pili, ambao wamepelekwa hospitali kwa matibabu.

Waliofariki dunia ni Alexander Paul, mwanafunzi wa darasa la tano, Ally Pongwe, mwanafunzi wa darasa la tatu na Hudhaifa Shafii, mwanafunzi wa darasa la tano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *