#HABARI: Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mageuzi anayoendelea kuyafanya kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwepo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Wametoa maoni hayo wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, mkoani Morogoro ambapo kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti, Najma Murtza Giga, wamefika kukagua Mradi wa Ukarabati wa Jengo la Kituo baada ya uchakavu wa mfumo wa umeme, uchakavu wa mfumo wa maji taka na maji safi, ubovu wa baadhi ya milango na madirisha, rangi ya jengo, sakafu ya ndani ya jengo,sehemu ya kuegeshea magari ya zimamoto na uokoaji, kuezeka na kuweka vigae eneo la wazi lililopo juu ya chumba cha habari ambapo gharama ya maboresho hayo ni Shilingi Milioni 299 ambazo fedha hiyo imetoka katika Bajeti ya Maendeleo ya Mwaka 2024/2025.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *