#MCHEZO: Serikali ya Senegal imetoa msimamo mkali sakata linalohusu Kombe la Africa Cup of Nations (AFCON), ikitangaza kuwa haitalirejesha kombe hilo kwa sasa hadi pale Court of Arbitration for Sport (CAS) itakapotoa uamuzi wake rasmi.
Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, kubadilisha picha yake ya wasifu kwenye mitandao ya kijamii, kitendo hicho kimetafsiriwa na wengi kama ujumbe wa kisiasa na kimkakati unaoashiria msimamo wa taifa hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa, Senegal tayari imelijulisha Confederation of African Football (CAF) kuwa haitarejesha kombe hilo hadi mchakato wa kisheria utakapokamilika, kwa kawaida mabingwa hutakiwa kulirejesha kombe kabla ya mashindano yanayofuata ili maandalizi ya toleo jipya yaanze.
Uamuzi huo unatazamwa kama hatua ya ujasiri inayochanganya siasa, sheria na michezo, huku wachambuzi wanasema hatua ya kuhusisha CAS inaonesha kuwa Senegal inataka suala hilo litazamwe katika misingi ya kisheria badala ya kiutawala pekee.
Hadi sasa, CAF haijatoa tamko rasmi kuhusu hatua zinazoweza kuchukuliwa iwapo kombe hilo halitarejeshwa kwa wakati.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.