Viongozi wa dini na serikali wamewaomba Watanzania kuendeleza ushirikiano, umoja na upendo waliouonesha katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, wakisisitiza umuhimu wa kudumisha maadili hayo hata baada ya kipindi hicho kumalizika.
Wakizungumza katika nyakati tofauti katika iftar iliyoandaliwa na Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Gdeita viongozi hao wamesema kuwa Ramadhani imekuwa ni chachu ya watu kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo kusaidiana, kutoa sadaka na kuwajali wenye uhitaji, hivyo ni vyema moyo huo ukaendelea kuwa sehemu ya maisha ya kila siku.
(Feed generated with FetchRSS)