#HABARI: Akizungumza leo Machi 20, 2026 katika hafla ya utiaji saini wa mradi wa barabara kuelekea uwanja wa AFCON 2027, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Paul Christian Makonda pamoja na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini wamesisitiza kuwa uwekezaji katika miundombinu ya barabara ni ajenda ya pamoja inayowaunganisha wananchi bila kujali tofauti za kisiasa. Wamesema kushuhudia utekelezaji wa miradi hiyo moja kwa moja huongeza imani na faraja kwa jamii.

Viongozi hao wameeleza kuwa wananchi wa Arusha wana mtazamo unaofanana kuhusu umuhimu wa barabara, wakiziona kama kipimo kikuu cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku wakisisitiza kuwa mahitaji ya miundombinu bora yanabaki kuwa kipaumbele kwa wote bila kujali itikadi za vyama.

Katika utekelezaji wake, mradi huo unatarajiwa kujenga kilometa 13 za barabara kwa viwango vya njia nne na mbili, huku mtandao wake ukifikia takribani kilometa 17.

Aidha, wametoa shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha fedha za mradi huo, wakieleza kuwa utaongeza kasi ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa wananchi wa Arusha.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *