#HABARI: Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limefanya ziara ya kijamii katika vituo vitatu vya watoto wenye mahitaji maalum jijini Dar es Salaam na kutoa misaada mbalimbali kwa ajili ya kuleta faraja.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Bi. Irene Gowelle, ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya uwajibikaji wa shirika kwa jamii, ikilenga kuwajengea watoto hao matumaini na ujasiri wa kuamini katika ndoto zao licha ya changamoto wanazokabiliana nazo.
Wamiliki na walezi wa vituo vya Umra Orphanage, CHAKUWAMA, na New Hope for Girls, wamelishukuru shirika hilo kwa kutoa msaada uliokuja wakati muafaka, hususan katika msimu huu wa sikukuu.
Bi. Rahma Juma na Bi. Nuru Mwegoha wamebainisha kuwa ujio wa TANESCO umeleta motisha mpya kwa watoto na kusaidia kupunguza changamoto za uendeshaji wa vituo hivyo, huku wakihimiza wadau wengine kuiga mfano huo wa upendo na mshikamano.
Mbali na kukidhi mahitaji ya msingi ya kila siku, TANESCO imesisitiza kuwa itaendelea kushirikiana na jamii inayozunguka maeneo yake ya kazi ili kuchangia katika ustawi wa pamoja wa taifa.
Shirika limetoa wito kwa makampuni na taasisi binafsi kujitokeza kusaidia makundi yenye uhitaji, likiamini kuwa ushirikiano huo ni nguzo muhimu katika kuhakikisha watoto yatima na wenye ulemavu wanapata huduma bora na kuishi maisha yenye utu na matumaini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.