
Watu kumi wamefariki katika kisa cha moto katika kiwanda cha kutengeneza vipuri vya magari nchini Korea Kusini, shirika la habari la Yonhap limeripoti leo Jumamosi, Machi 21. Wengine hamsini na tisa wamejeruhiwa katika moto huo, uliotokea siku ya Ijumaa huko Daejeon (Korea ya Kati), shirika hilo limesema, likinukuu mamlaka za eneo hilo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Moto katika kiwanda cha kutengeneza vipuri vya magari huko Daejeon, Korea Kusini, ulisababisha vifo vya watu kumi na 59 kujeruhiwa Ijumaa. Juhudi za uokoaji zinaendelea kutokana na uwepo wa vifaa vya kulipuka.
Moto huo ulizuka yapata saa 7:00 mchana (11:00 alfajiri saa za Paris) huku wafanyakazi 170 wakiwa ndani ya eneo la kiwanda. Mazingira halisi ya moto huo bado hayajajulikana kwa sasa.
Uwepo wa vifaa vya kulipuka
Idara ya huduma za dharura zilikumbana na ugumu wa kujibu haraka kutokana na hatari ya jengo kuanguka, jambo lililochelewesha ufikiaji wa wazima moto katika baadhi ya maeneo ya kiwanda.
Kituo hicho pia kilikuwa na takriban kilo 200 za sodiamu, dutu inayoweza kulipuka ikiwa itashughulikiwa vibaya, kulingana na Yonhap. Rais wa Korea Kusini Lee Jae-myung ameagiza kutumwakwa wafanyakazi na vifaa vyote vilivyopatikana kwa ajili ya shughuli za uokoaji.