Serikali imesema inaendelea na mazungumzo na mataifa yanayozalisha mafuta ili kupunguza athari za uwezekano wa upungufu wa nishati nchini, kufuatia kuendelea kwa mgogoro katika eneo la Mashariki ya Kati.

Akizungumza jijini Mwanza, Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unaendelea kupitia vyanzo mbadala.

Amesema licha ya jitihada hizo, wananchi wanapaswa kujiandaa na mabadiliko ya bei za mafuta kutokana na athari za biashara za kimataifa zinazosababishwa na mgogoro huo.

✍ Innocent Aloyce
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *