Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya Musalia Mudavadi, amesema Wakenya waliosajiliwa kupigana katika vita vya Ukraine kwa niaba ya Urusi watasamehewa wakati watakaporejea nyumbani.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangazo lake limekuja baada ya kuzuru Moscow wiki iliyopita katika juhudi za Nairobi kujaribu kutafuta suluhu la raia wake kusajiliwa katika vita vya Ukraine.

Katika kikao chake na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, walikubaliana kwamba raia wengine wa Kenya hawatosajiliwa katika vita hivyo.

Kulingana na sheria za kenya, ni kinyume cha sheria kwa raia wake kusajiliwa kama mwanajeshi katika vikosi vya kigeni, kosa ambalo mhusika anaweza kufungwa jela miaka 10.

Sergei Lavrov- Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi na mwenzake wa Kenya Musalia Mudavadi.
Sergei Lavrov- Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi na mwenzake wa Kenya Musalia Mudavadi. via REUTERS – Tatyana Makeyeva

Kwa mujibu wa Wizara ya mambo ya nje,  Wakenya 252 wanapigana katika vita vya Ukraine, ambapo walianza kusajiliwa miezi sita iliopita, nchi nyengine za Afrika zikiripoti pia raia wake kusajiliwa kwenye vita hivyo.

Baadhi ya Wakenya waliorejea wamedai walidaganywa kwamba wangepewa kazi zenye mishaara minono kabla ya kujipata vitani, Nairobi ikiwa tayari imefunga baadhi ya ofisi zilizohusika kuwasajili Wakenya hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *