Nchini Kenya, mvua kubwa inaendelea kusababisha uharibifu mkubwa kote nchini. Watu themanini na mmoja wamepoteza maisha yao kutokana na mafuriko tangu mwanzoni mwa mwezi Machi, kulingana na takwimu za hivi karibuni za polisi zilizotolewa siku ya Jumapili, Machi 22. Zaidi ya familia 2,000 zimeyakimbia makazi yao.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Nairobi, Albane Thirouard

Nairobi inabaki kuwa eneo lililoathiriwa zaidi ikirekodi  waathiriwa 37. Kwa utabiri wa mvua kubwa kwa wikendi hii na inatarajiwa kuendelea hadi Machi 23, wakazi wanaoishi kando ya mito ya mji mkuu wanaendelea kuwa macho.

Katika eneo lenye wakazi duni la Mukuru Kayaba jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, Mto Ngong ulivunja kingo zake usiku wa Machi 6 kuamkia Machi 7, na tena Machi 14 kuamkia Machi 15, na kusababisha mafuriko makubwa. Dorothy Mathai aliona nyumba yake ikikumbwa na mafuriko mara mbili. Alasiri ya Machi 22, hakuna mafuriko mapya yaliyoripotiwa nyumbani kwake, lakini aliendelea kuwa macho. “Hili ni begi nililoandaa kwa ajili ya kuondoka kwa dharura. Nimeweka nguo zangu za kanisani na begi la shule. Ninaogopa; siwezi kulala. Mimi huangalia mto mara kwa mara ili kuona kama kiwango kinaongezeka.”

Kuongezeka kwa kiwango cha maji katika bwawa pia kunatishia kuvunja Bwawa la Nairobi, na kusababisha hatari ya mafuriko kwa jamii zilizo chini ya mto. Mukuru Kayaba iko hatarini. Clinton Kissia ana wasiwasi. Duka lake anakofanyia biashara ya mtandaoni na nyumba yake tayari zimejaa maji kutokana na mafuriko. “Nilikuwa na vifaa vinne vya michezo, televisheni nne, kompyuta mbili, na printa. Kila kitu kiliharibiwa. Kama naweza kukusanya fedha zinazohitajika, naweza kuhamia kwingine, lakini baada ya uharibifu nilioupata, ni vigumu. Serikali inapaswa kuwa na mpango, iwe ni kutuhamisha au kufungua bwawa ili kuruhusu maji yatiririke.” “Wanapaswa kupanga vyema.”

Utata unaongezeka dhidi ya mamlaka. Gavana wa mji mkuu ameamuru tu kubomolewa kwa ujenzi haramu kando ya kingo za mito, ambao unalaumiwa kwa kupunguza mtiririko wa maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *