Masanduku yenye pesa taslimu yakamatwa na mamilioni ya dola yamekosekana. Fedha taslimu zinasambaa kwa uhuru nchii Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo karibu dola milioni mbili zilikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ndjili katika mji mkuu, Kinshasa. Waziri wa Sheria ameamuru uchunguzi ufanyike na kuonya kuhusu hatari ya kutoweka kwa fedha hizi zilizokamatwa. Kashfa hii imezua utata mkubwa nchini na kuzua maswali kuhusu utawala.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Pascal Mulegwa

Tukio hilo linaripotiwa kutokea siku ya Jumamosi, Machi 21, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ndjili huko Kinshasa, mji mkuu wa DRC. Wakati wa ukaguzi wa kawaida wa ndege ya abiria inayofanya safari za kimataifa, idara za usalama ziligundua kiasi kikubwa cha pesa taslimu kilichofichwa katika masanduku mawili.

Kwa jumla, dola milioni 1.9 za Marekani zilikamatwa, zikiwa zimeunganishwa kwa uangalifu katika marundo. Utambulisho wa mmiliki wa masanduku bado haujawekwa wazi. Waziri wa Sheria Guillaume Ngefa, katika taarifa yake, alirejelea taarifa inayoonyesha “ushughulikiaji usio wa kawaida, au hata ugawanaji, wa fedha hizi.”

Alimwamuru Mwanasheria Mkuu kuchukua hatua mara moja ya kushughulikia kesi hiyo, bila ubaguzi. Fedha hizo zitahifadhiwa, wakiwepo maafisa wa polisi wa mahakama, pamoja na ripoti ya kina inayoelezea mazingira ya kukamatwa kwa fedha hizo na kuwatambua watu waliohusika. Kisha zitawekwa katika Benki Kuu ya Kongo, huku hati hizo zikipelekwa kwa Kitengo cha Kitaifa cha Ujasusi wa Fedha.

Hii sio kashfa pekee ya aina yake inayosambaa kwa sasa. Mapema wiki iliyopita, video iliyorekodiwa katika chumba cha hoteli cha Kinshasa ilivuja mtandaoni. Picha hizo zinaonyesha vifurushi vingi vya dola, vikiambatana na maoni yanayoashiria fedha hizo zilitoka Benki Kuu na zilikusudiwa kwa rushwa. Hali inayoanzisha mjadala kuhusu utawala na utakatishaji fedha nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *