Mkuu wa Shirika la Nishati la Kimataifa ameonya ulimwengu kuhusu mgogoro mbaya zaidi wa nishati kwa miongo kadhaa, ikiwa hakutachukuliwa hatua za haraka kusitisha mgogoro huo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Dunia inaweza kukabiliwa na mgogoro wake mbaya zaidi wa nishati katika miongo kadhaa, ameonya mkuu wa Shirika la Nishati la Kimataifa. “Hakuna nchi” itakayoepuka athari za mgogoro wa nishati ulnaosababishwa na vita vya Mashariki ya Kati, amesema Fatih Birol, mkurugenzi wa Shirika la Nishati la Kimataifa (IEA), leo Jumatatu, Machi 23, akielezea kama “tishio kubwa” kwa uchumi wa dunia.

“Hadi leo, tumepoteza mapipa milioni 11 kwa siku, zaidi ya migogoro miwili mikubwa ya mafuta kwa pamoja,” ameambia waandishi wa Habari huko Canberra, akimaanisha migogoro ya miaka ya 1970. “Wakati huo, kwa kila moja ya migogoro hiyo, dunia ilipoteza takriban mapipa milioni tano kwa siku, kwa hivyo, tukiongeza hayo mawili pamoja, mapipa milioni 10 kwa siku,” Birol ameongeza.

“Hakuna nchi itakayokuwa salama kutokana na athari za mgogoro huu ikiwa utaendelea katika njia yake ya sasa. Kwa hivyo, hatua za kimataifa ni muhimu,” aesema. Kulingana na Fatih Birol, angalau miundombinu 40 ya nishati imeharibiwa “vikali au vibaya sana” kutokana na mzozo katika Mashariki ya Kati, katika nchi tisa.

Hayo yanajiri wakati Iran ilitishia siku ya Jumapili, Machi 22, kushambulia miundombinu muhimu katika eneo hilo na kufunga kabisa Mlango-Bahari wa Hormuz, ikijibu mara moja makataa ya Donald Trump ya kufungua tena mlango-bahari huo ndani ya saa 48. 

Kwa upande wake, Israel inapaswa kutarajia “wiki kadhaa zaidi za mapigano” dhidi ya Hezbollah ya Lebanon na Iran, alionya msemaji wa jeshi la Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *