
Katika kujibu hatua ya hivi karibuni ya viongozi wa Al-Azhar, Chuo Kikuu cha Kidini cha nchini Misri ya kulaani hatua ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kulipiza kisasi dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani katika ardhi za nchi za Kiarabu za Ghuba ya Ujemi, viongozi tofauti wa kidini akiwemo Ayatullah Sheikh Muhammad Jawad Fadhil Lankarani wametoa taarifa wakikosoa vikali hatua hiyo ya kibaguzi ya wanazuoni wa Al- Azhar.
Ikiwa ni katika kujibu hatua ya hivi karibuni ya viongozi wa Al-Azhar, Chuo Kikuu cha Kidini cha nchini Misri ya kulaani hatua ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kulipiza kisasi dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani katika ardhi za nchi za Kiarabu za Ghuba ya Ujemi, baada ya vituo hivyo kutumiwa na Marekani na utawala haramu wa Israel kuishambulia Iran na kuua kigaidi viongozi wake wa ngazi za juu, viongozi tofauti wa kidini akiwemo Ayatullah Sheikh Muhammad Jawad Fadhil Lankarani wametoa taarifa wakikosoa vikali hatua hiyo ya kibaguzi na ya upendeleo ya wanazuoni wa Al- Azhar. Ifuatayo ni taarifa kamili ya Ayatullah Sheikh Muhammad Jawad Lankarani kuhusu hatua hiyo isiyofaa ya wanazuoni wa Al-Azhar:
Ifuatayo ni taarifa kamili ya Ayatullah Sheikh Muhammad Jawad Lankarani kuhusu hatua hiyo isiyofaa ya wanazuoni wa Al-Azhar:
Bismillahir Rahmanir Rahim
Kwa Umma wa Kiislamu na wanazuoni wa Kiislamu, hususan wanazuoni waheshimiwa wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar
Salaam Alaykum
Nimeona taarifa ya kushangaza na isiyotarajiwa kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar. Kwa kweli siwezi kukubali kwamba taasisi hii, ambayo ina historia hii yote ya kielimu na kuwa huru, inaweza kutoa taarifa kama hii leo. Pamoja na kuwa hatusahau misimamo madhubuti na sahihi ya Al-Azhar kuhusiana na suala la Palestina na Ghaza, lakini taarifa hii imeibua maswali muhimu katika fikra za wanazuoni wote. Je, Al-Azhar haijiulizi ni kwa nini serikali zinazojiita kuwa za Kiislamu katika eneo zimeruhusu ardhi na anga zao kutumiwa na makafiri na Mayahudi? Je, haijiulizi ni nini lengo la Marekani na Israel la kuwepo na kudhibiti eneo hili? Je, haitafakari namna wanavyotaka kupora rasilimali za Waislamu na kuharibu idadi (maisha) na mali zao?
Je! Al-Azhar imesahau Aya chungu nzima za Qur’ani tukufu ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anawakataza Waislamu kukubali satwa na udhibiti wa makafiri na Mayahudi? Kwa kuzingatia Aya tukufu inayosema, “Na anayekushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyokushambulieni,” je, Iran ya Kiislamu, ambayo imefanyiwa uchokozi wa kikatili na Marekani na Israel kupitia vituo vyao vya kijeshi katika eneo, haina haki ya kujitetea? Kwa kutilia maanani Aya tukufu inayosema, “Na mkilipiza kisasi basi lipizeni sawa na vile mlivyoadhibiwa,” je, Iran haipaswi kulipiza kisasi? Je, kwa kuzingatia Aya tukufu inayosema, “Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa – na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia,” Iran hairuhusiwi kulipiza kisasi?
Je, hawajasoma au wamesahau Aya tukufu inayosema: “Enyi mlioamini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyokujieni? Je, hawaamini Aya tukufu inayosema: “Enyi mlioamini! Msiwafanye rafiki zenu watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia? Je, hawapasi kuifanya Aya hii tukufu inayosema: “Huwakuti watu wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake,” kuwa kipimo cha vitendo na kauli zao? Je, taarifa hii inaendana na Hadith mashuhuri inayokubaliwa na pande zote mbili, yaani Hadithi ya Al-Thaqalayn, au ni kinyume kabisa na malengo ya Qurani Tukufu na kizazi cha Mtume?
Je, Al-Azhar imesahau misingi ya fiqhi ambayo inakubaliwa na Waislamu wote? Je, si vitabu vya fiqhi vinasema kwamba Waislamu wanaowasaidia makafiri wafanikiwe dhidi ya kundi jingine la Waislamu wao pia wanahesabiwa kuwa ni makafiri, na ikiwa watakuwa ngao ya makafiri basi wao pia waangamizwe? Lau Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) angekuwepo katika zama zetu hizi, je, angeiunga mkono Marekani, Israel, na serikali za eneo ambazo zimezifanya ardhi za Kiislamu kuwa vituo vyao vya kijeshi, au bila shaka angetetea taifa la Kiislamu la Iran, ambalo limedhulumiwa na kuvamiwa na maadui?
Hata ukiachilia mbali mantiki ya Qurani na Sunnah, na kuwauliza watu walio huru duniani kwamba je, kimantiki Iran ilipasa kufanya nini baada ya kukabiliwa na mashambulizi haya ya serikali haini za eneo? Je, haikupasa kutetea roho, damu na heshima ya Waislamu katika nchi hii? Je, hamukuona katika siku ya kwanza ya vita namna maadui hawa walivyoshambulia shule ya Shajarah Tayyiba huko Minab na kuwauwa shahidi zaidi ya watoto 160 wasio na hatia? Mnaegemea na kuutetea upande wa serikali za eneo na wakati huo huo kuilaani Iran kwa kutegemea Aya gani ya Qurani au Hadithi au kwa msingi wa hoja gani ya kimantiki na busara? Kwa nini hamukusoma Aya tukufu inayosema “Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha kuuawa isipokuwa kwa haki,” katika kuwakemea makafiri na nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi? Kwa nini nyinyi wanazuoni wa Al-Azhar hamkusema lolote baada ya kuuawa shahidi kidhulma Kiongozi wa Waislamu nchini Iran, ambaye siku zote alikuwa mhubiri mkubwa wa utukufu wa Uislamu na Waislamu na kuwaletea heshima na utukufu Waislamu wote duniani?!
Je, hamdhani kwamba kwa taarifa hii mnadhoofisha na kuhafifisha imani ya Waislamu duniani kwa taasisi hii (Al-Azhar)?
Ninawausia wanazuoni wa Ulimwengu wa Kiislamu, hususan wa Al-Azhar, wazingatie vizuri na kwa umakini hali ya sasa ya ulimwengu na watekeleze majukumu yao kwa msingi wa wajibu wao wa kidini na kisheria, na sio kwa msingi wa kuwaridhisha viongozi wa ukafiri na uistikbari na vibaraka wao katika eneo. Hilo litawawezesha kufanikiwa na kupata radhi za Mwenyezi Mungu, Mtume Mtukufu wa Uislamu, mawalii wa Mwenyezi Mungu, Waislamu na watu wote walio huru duniani. Mwenyezi Mungu awaepushie mbali kuwa miongoni mwa makusudio ya Aya tukufu inayosema “Hakika wale wanaoficha aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu, wakanunua kwacho thamani ndogo.”
“Mola wetu Mlezi! Tusamehe madhambi yetu na ubadhirifu wetu katika mambo yetu, na usimamishe imara miguu yetu, na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri.”
Qum – Chuo cha Kidini
Muhammad Jawad Fadhil Lankarani
28 Ramadhani 1447