Kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta kinachomilikiwa na tajiri namba moja barani Afrika Mnigeria, Aliko Dangote, kimethibitisha kuanza kusafirisha mafuta katika mataifa mbalimbali ya Afrika, baada ya bei ya bidhaa hiyo kupanda kwenye soko la kimataifa kwa sababu ya vita vya Mashariki ya Kati.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Vita vinavyoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati kwa wiki tatu sasa, imetatiza safari za meli za mafuta, baada ya Iran kufunga mlango wa Bahari wa Hormuz, hali ambayo imetatiza safari za meli ya mafuta.

Kiwanda hicho Dangote chenye makao yake jijini Lagos, kimesema, tayari imeuza tani 456,000 za mafuta kwa nchi za Ivory Coast, Cameroon, Tanzania, Ghana  na Togo.

Kiwanda cha Dangote kimeanza kusafirisha mafuta katika baadhi ya nchi za Afrika kutokana na vita vya mashariki ya kati.
Kiwanda cha Dangote kimeanza kusafirisha mafuta katika baadhi ya nchi za Afrika kutokana na vita vya mashariki ya kati. REUTERS – Sodiq Adelakun

Kwa siku, kiwanda hicho kuzalisha mapipa 650,000 ya mafuta kila siku, kiwango ambacho kinatosheleza soko la ndani na nje, na hatua ya kuanza kusafirisha bidhaa hiyo katika nchi za Afrika, inalenga kusaidia kuimarisha sekta ya nishati katika mataifa hayo.

Barani Afrika, Nigeria ndio nchi ya kwanza inayozalisha mafuta, lakini nchi hiyo bado inakabiliwa na bei kubwa. Mfano Lita moja ya Petroli imeongezeka kutoka Naira 830 hadi 1,300 jijini Lagos.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *