
Mapigano makali yameripotiwa mapema Jumatatu nchini DRC, baada ya waasi wa AFC/M23 kuvamia ngome ya wapiganaji wa Wazalendo eneo la Kazinga, wilayani Masisi mkoani Kivu Kaskazini.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Makabiliano hayo, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, yalianza mida ya saa kumi na moja Alfajiri, baada ya waasi wa M23 kuvamia eneo la Kazinga ambalo kwa sasa linadhibitiwa na Wazalendo.
Wenyeji wa eneo hilo wanadai mashambulio hayo ya M23 yanalenga kuwaondoa vijana wa wazalendo eneo hilo na kulidhibiti tena.
Mapigano haya mapya yanadhihirisha wazi utovu wa usalama unaoendelea kulikumba eneo la Masisi, eneo ambalo limeendelea kushuhudia vita vikali kati ya waasi wa M23 na jeshi la Serikali, ambalo linasaidiwa na vijana wa wazalendo, raia wa eneo hilo wakiripotiwa kuendelea kulikimbia kutokana na utovu wa usalama
Mapigano haya yanakuja licha ya kuwepo kwa makubaliano mapya wiki iliyopita kati ya Rwanda na DRC, ili kuchukua hatua za makusudi kusitisha vita mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mwaka wa pili sasa, miji ya Goma na Bukavu, inadhibitiwa na waasi wa M23/AFC.