Uchaguzi wa Uganda wa Januari 15 mwaka huu, sasa umeenda kupingwa katika mahakama ya Afrika Mashariki iliyoko jijini Arusha nchini Tanzania, ambapo chama cha wanasheria wa Uganda na kile cha Afrika mashariki wanazituhumu Idara za Serikali kwa kukiua misingi ya kidemokrasia na haki za raia.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika kesi ambayo ilifunguliwa Machi 16 na taasisi hizi mbili za kisheria, zinadai tume ya uchaguzi ya Uganda Pamoja na mwanasheria mkuu wa Serikali waliharibuj mchakato wa uchaguzi kinyume na mkataba wa jumuiya.

Wanasheria hao wamedai kuwa, wakati na baada ya uchaguzi huo ambao matokeo yake yalitangazwa Januari 17, Idara za Serikali zilijihusisha na vitendo ambavyo viliharibu uhalali wa kura iliyofanyika, ikiwemo uteuzi wa makamishna wa tume, kushindwa kufanya marekebisho ya sheria za uchaguzi na utata wa daftari la wapiga kura.

Malalamiko mengine yanahusu tume kushindwa kushirikisha wadai ilipofanya marekebisho ya kanuni za uchaguzi, kukataa kutoa vibali kwa waangalizi wa ndani nan je, ubaguzi dhidi ya wapinzani na vurugu dhidi ya wagombea na mawakala wao.

Katika maombi yao, wanasheria hawa wanataka mahakama itamke kuwa uchaguzi wa Januari 15 ulishindwa kukidhi vigezo vya kisheria, misingi ya demokrasia na kwamba matokeo yake ni batili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *