Rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila, amemkosoa mrithi wake rais Felix Tshisekedi, kiongozi huyu wa zamani akitaka kufanyika kwa mabadiliko ya uongozi kwenye taifa lake, matamshi aliyoyatoa katika mahojiano ya kwanza na jarida la Ubelgiji, La Libre Belgique.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano hayo, amerejelea mazungumzo ya amani yaliyofanyika wakati wa utawala wake, na ambayo amesema yalisaidia pakubwa kuliokoa taifa hilo dhidi ya migogoro kadhaa, ikiwemo ya kisiasa na kijamii.

Kabila ambaye amehukumiwa kunyongwa kutokana na kuhusika kwake kwenye mzozo wa mashariki mwa nchi hiyo, pia amehoji uhalali wa mazungumzo ya kitaifa yaliyoanzishwa na rais Tshisedi.

Aidha Kabila, amemtaja rais Félix Tshisekedi kuwa mchochezi na mpenda vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi hiyo, akikosoa michakato ya utafutaji wa amani inayoendelea.

Akijibu swali linalohusu mabadiliko ya katiba, Kabila amesema tatizo kubwa kwenye nchi yake ni utawala bora, ukosefu wa maono, huku akienda mbali zaidi na kudai kuwa Katiba iliopo imekanyagwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *