#HABARI: Ndege ya kijeshi aina ya C-130 Hercules mali ya Jeshi la Anga la Colombia imeanguka siku Jumatatu katika eneo la Puerto Leguízamo, mkoa wa Putumayo, ikiwa na watu 128 ndani yake.
Ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya kupaa, takriban kilomita 1.5 kutoka uwanja wa ndege, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 66 huku wengine wanne wakiwa hawajulikani walipo, kwa mujibu wa taarifa za awali za kijeshi na viongozi wa mkoa huo.
Licha ya Rais Gustavo Petro kueleza awali kuwa wanajeshi vijana 83 walikuwa hai, hali imebadilika huku Waziri wa Ulinzi, Pedro Sánchez, akithibitisha kuwa majeruhi kadhaa wamepelekwa hospitalini kwa matibabu ya dharura.
Mamlaka bado zinachakata takwimu rasmi za majeruhi na vifo, huku kukiwa na hofu kuwa idadi ya waliopoteza maisha inaweza kuongezeka kutokana na ukubwa wa ajali hiyo iliyotokea mpakani mwa Colombia na Peru.
Serikali ya Colombia imetangaza kuanza kwa taratibu za kusaidia familia za wahanga pamoja na kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha ajali hiyo ya kushtua.
Kamanda wa Jeshi la Anga, Carlos Fernando Silva Rueda, amesisitiza kuwa timu za uokoaji bado zipo eneo la tukio, huku dunia ikisubiri taarifa kamili kuhusu hatima ya abiria na wafanyakazi waliohusika katika maafa hayo ya anga.
#BBCSwahili
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)