
Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu mauaji yanayotekelezwa na utawala huo dhidi ya raia wa Palestina na Lebanon. Taarifa ya IRGC imesema jeshi katili la Israel limevuka mistari yote myekundu katika mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina na Walebanon.
Kwa mujibu wa kitengo cha habari za ulinzi cha Shirika la Habari la Tasnim, taarifa namba 46 ya Operesheni “Ahadi ya Kweli 4” iliyotolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imesema yafuatayo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
“Na kwa nini hampigani katika njia ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya wanaodhulumiwa miongoni mwa wanaume, wanawake na watoto.”
Jeshi la utawala wa Kizayuni linalojulikana kwa mauaji ya watoto, kwa kutumia vibaya hali ya vita katika eneo hili na kwa kuchukua fursa ya kuelekezwa kwa vyombo vya habari kwenye vita vilivyolazimishwa na Marekani na utawala huo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, limefanya uhalifu mkubwa wa kivita dhidi ya raia wasiokuwa na hatia katika Lebanon na Palestina, na katika vitendo vya mauaji ya halaiki limevuka mipaka yote ya kibinadamu na kisheria. Kuendelea kwa hali hii hakukubaliki.
Tunalionya jeshi litendalo jina la utawala huo kwamba endapo uhalifu dhidi ya raia wa Lebanon na Palestina utaendelea, maeneo ya mkusanyiko wa vikosi vya adui katika kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na pia katika ukanda wa Gaza yatakuwa chini ya mashambulizi mazito ya makombora na ndege zisizo na rubani za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu bila kujali hali yoyote.
Na ushindi hauji isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mwenye hekima.