Kamanda wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesisitiza udharura wa kuendelezwa vita hadi Iran itakapolipwa gharama kamili za hasara zilizosababishwa na adui Mmarekani na Mzayuni.

Brigedia Jenerali Mohsin Rezaei ambaye ni mjumbe katika Baraza la Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu hapa nchini amezungumzia vitisho vya Donald Trump vya kushambulia miundombinu ya umeme ya Iran na kusema: “Tunamwambia Trump kwamba kama utapiga hatutalipiza kisasi cha jicho kwa jicho, bali kichwa kwa jicho na utaghariki katika maji ya Ghuba ya Uajemi.”

Brigedia Jenerali Mohsin Rezaei amesisitiza udharura wa kuendelezwa vita hadi pale Iran itakapolipwa hasara zote za vita, kuondolewa vikwazo vyote vya kiuchumi na kutolewa dhamana ya kisheria ya kimataifa kwamba Marekani haitaingilia tena mambo ya ndani ya Iran.

Mjumbe wa Baraza la Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu nchini Iran amesema hivi karibuni kutashuhudiwa mpasuko mkubwa kati ya Marekani na utawala haramu wa Israel na kuongoza kuwa: Netanyahu anamburuta Trump, na tangu mwanzoni mwa vita vya sasa mipango ya vita ya wawili hawa ilikuwa tofauti.

Brigedia Jenerali Mohsen Rezaie amesema, awali Marekani ilitaka kuanzisha vita vya muda mfupi lakini mtazamo wa Netanyahu ndio unaotekelezwa kwani Trump alitaka kukomesha vita katika siku ya 12.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *