MOROGORO: MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amewaonya wananchi wa mkoa huo wanaotumia vyandarua kwa malengo tofauti zikiwemo kufugia kuku, kuzungushia bustani na kuvulia samaki badala ya matumizi sahihi ya  kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa malaria.

Malima ametoa onyo hilo wakati katika uzindua kampeni ya usambazaji na ugawaji wa vyandarua vyenye dawa uliofanyika mkoani humo yenye kauli mbiu: “Ziro Malaria inaanza na Mimi” Nachukua Hatua Kuitokomeza.

Amesema imebainika kuwa baada ya kugawiwa vyandarua ili wazitumie kwa lengo lililokusudiwa, imebainika baadhi yao wanazitumia kufugia kuku au kuvulia samaki na hivyo kikwanzo cha mapambano ya  kutokomeza maambuziki ya  malaria nchini

“Lazima tuwe wakali katika jambo hilo , tufuatilie kaya kuhusu matumizi yake ili kudhibiti maambukizi ya malaria kwa jamii,“amesema Malima.

Amesema  kuwa Morogoro imejipanga kuwa  moja ya Mikoa kinara kwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.“Jukumu  la kupambana na malaria si la Serikali pekee, bali ni la mwananchi wote,” amesema Malima

Mkuu wa mkoa aamewataka wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia ipasavyo utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa matumizi ya vyandarua pamoja na kuchukua hatua za kudhibiti mazalia ya mbu, ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na kuleta matokeo chanya.

Katika ugawaji huo  jumla ya vyandarua vyenye dawa 1,686,933  zimetolewa na kusambazwa  katika halmashauri saba kati ya tisa  ambazo zimebainika na maambukizi ya juu ya malaria.

Vyandarua yenye dawa vitasabazwa katika kata 165 , vijiji 656 na vituo vya kugawia 1,047 na zimetolewa bila malipo na ni sehemu ya mkakati wa kupunguza maambukizi ya malaria hususan kwa makundi yaliyo hatarini ambayo ni watoto na wanawake wajawazito.

Naye  Mkurugenzi wa Usimamizi wa Bohari ya Dawa (MSD), Hassan Ibrahim, amesema  katika kipindi cha mwaka 2019 hadi 2020, jumla ya halmashauri 50 nchini zilipatiwa vyandarua zaidi ya milioni 16, hatua iliyonesha dhamira ya Serikali katika kupambana na malaria kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wake Mratibu na Mdhibiti wa Malaria kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Stella Kajange, amesema  Wizara ya Afya kwa kushirikiana na  Tamisemi imeandaa mwongozo maalum wa kitaifa wa mapambano dhidi ya malari.

Kajange amesema  kuwa jitihada hizo zinahitaji ushirikiano wa sekta mbalimbali, kwani mapambano dhidi ya malaria si jukumu la Wizara ya Afya pekee bali la jamii nzima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *