Marekani imewasilisha kwa Iran mpango wa pointi 15 ili kujaribu kukomesha mzozo unaoendelea, ambao kwa mfano, uinaitaka Tehran kukabidhi mafuta yake yote ya nyuklia yaliyorutubishwa na kuacha wazi Mlango-Bahari wa Hormuz, vyombo kadhaa vya habari vimeripoti siku ya Jumanne.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Gazeti la New York Times na kituo cha televisheni cha Israel, Channel 12, vimeripoti kwamba utawala wa Trump uliwasilisha madai yake kwa Iran kupitia Pakistan, ambayo inadumisha uhusiano mzuri na pande zote mbili.

Kulingana na vyanzo vitatu visivyojulikana vilivyonukuliwa na Channel 12, wapatanishi wa Marekani—mjumbe maalum Steve Witkoff na mkwe wa Donald Trump Jared Kushner—wanapendekeza kusitisha mapigano kwa kipindi cha mwezi mmoja, na kuipa mamlaka ya Iran muda wa kuzingatia madai yao.

Kati ya pointi 15 zilizotolewa, tano za kwanza zinahusu sekta ya nyuklia: Washington inadai kwamba Iran kamwe isijaribu kupata silaha za nyuklia, na Tehran isalimishe mafuta yake yote yaliyorutubishwa ifikapo tarehe itakayokubaliwa na pande hizo mbili, na kwamba vituo kadhaa vikubwa vya nyuklia vibomolewe.

Iran lazima pia ikomeshe usaidizi wake kwa washirika wake na kusitisha ufadhili kwa makundi yenye silaha kama Hezbollah na Hamas. Mipaka itawekwa kwenye idadi ya makombora ambayo nchi hii inaweza kumiliki na umbali wa masafa yake.

Hata hivyo, Mlango-Bahari wa Hormuz, ambao takriban 20% ya hidrokaboni zinazopita duniani, lazima ubaki wazi kwa usafiri wa baharini.

Kwa kubadilishana, Iran itaondolewa vikwazo vya kimataifa dhidi yake na kuungwa mkono kwa mpango wake wa nyuklia kwa malengo ya kiraia. Mpango huo hautaji mabadiliko ya utawala nchini Iran.

Hata ivyo Ikulu ya White House na Wizara ya Mambo ya Nje havikusema hochote kuhusiana na hilo. Siku ya Jumanne, Donald Trump alionyesha matumaini kuhusu uwezekano wa kufikia makubaliano na Tehran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *