SERIKALI chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuleta mabadiliko chanya kupitia elimu ya ufundi stadi. Mafanikio hayo yanaonekana katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sikonge kilichopo Tabora, ambapo takriban vijana 100 wamepata mafunzo ya fani mbalimbali ikiwemo umeme, ushonaji, uchomeleaji na ufundi bomba.

Kwa mujibu wa Mkuu wa chuo hicho, Gaston Chiwalanga, hatua hiyo imewezekana baada ya serikali kutoa shilingi milioni 50 kugharamia mafunzo hayo.Mbali na elimu, vijana hao pia wanapatiwa huduma muhimu kama chakula na malazi bure, jambo linalowawezesha kujikita kikamilifu katika kujifunza na kujenga mustakabali wao.

Mpango huu umeleta matumaini mapya kwa vijana wengi waliokuwa na changamoto za kifedha, na sasa unawapa nafasi ya kujitegemea na kushiriki katika kukuza uchumi wao binafsi pamoja na taifa kwa ujumla. SOMA : Wafungwa 73 wahitimu mafunzo ufundi stadi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *