
Licha ya mapendekezo 15 ya Rais Trump yaliotumwa kwa Iran kumaliza mzozo wa mashariki ya kati kutowekwa wazi, vyombo vya habari vya Marekani na Israeli vimechapisha baadhi ya mapendekezo hayo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa shirika la habari la Israeli Channel 12, mpango wa Rais Trump unajumuisha
-Shuguli katika vinu vya nyukilia vya Natanz, Fordow na Isfahan zitasitishwa na vinu hivyo kuharibiwa.
-Shirika la nishati ya Atomiki (IAEA) litapewa nafasi ya kufuatilia kwa uwazi shughuli zinazohusiana na nyukilia nchini Iran.
-Iran itaacha kuyahami makundi yenye silaha kwenye ukanda pamoja na kusitisha ufadhili wake kwa makundi hayo yenye silaha.
-Tehran itaharibu silaha zote za nyukilia ambazo tayari imejenga.
-Tehran pia itahitajika kuonyesha nia ya kutorejelea juhudi za kumiliki silaha za nyukilia.
-Iran pia haitoruhusiwa kurutubisha urani katika ardhi yake na ile ambayo tayari imerutubishwa itawasilishwa kwa shirika la nishati ya Atomiki
-Mfereji wa Hormuz utasalia kuwa umefunguliwa na kuruhusu shughuli kuendelea bila vikwazo.
-Uamuzi kuhusu makombora ya Iran utajadiliwa baadaye lakini yatatumika tu kwa ajili ya Iran yenyewe kujilinda na hayatakuwa na vipimo vya umbali ambao yanaweza kufika.
Iran itapata nini kwenye makubaliano hayo?
-Marekani itaisaidia Tehran kujenga mradi wa nyukilia wa kiraia katika kinu cha nyukilia cha Bushehr kwa ajili ya uzalishaji wa umeme.
-Vikwazo vyote dhidi ya Iran vitaondolewa.
-Tishio la kutangazwa vikwazo vipya dhidi ya Iran pia vitandolewa.
Kando na hayo kuna ripoti kwamba kutakuwa na kipindi cha mwezi mmoja cha usitishaji wa mapigano wakati mapendekezo haya yakijadiliwa. Washington yenyewe haijaweza kuweka wazi mapendekezo licha kutangazwa kwenye vyombo vyake vya habari.