#HABARI: Watumishi kutoka Wizara ya Elimu na Ofisi ya Rais – TAMISEMI wameanza kujengewa uwezo mjini Morogoro kuhusu matumizi sahihi ya takwimu ili kutatua changamoto ya ucheleweshaji wa miradi ya maendeleo nchini.
Mafunzo hayo yanayotolewa na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), yanalenga kuziba pengo kati ya mipango ya Serikali na utekelezaji wake kwa kuwapa watumishi mbinu za kisasa za ufuatiliaji na tathmini ya rasilimali za umma.
Mkuu wa EASTC, Dkt. Tumaini Katunzi, amesisitiza kuwa takwimu sahihi ni nyenzo muhimu katika kufikia malengo ya kitaifa kwa ufanisi, huku mratibu wa programu hiyo, Kidney Chilingo, akibainisha kuwa washiriki wanapata ujuzi wa vitendo.
Elimu hii inatarajiwa kuleta mapinduzi katika maamuzi ya kisera na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa tija zaidi ili kuleta mabadiliko chanya ndani ya taasisi za umma.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)