Israel inasema imemuua Alireza Tangsiri, Kamanda wa kikosi cha majini cha jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Iran, katika mashambulizi mazito yaliyofanyika usiku wa kuamkia Alhamisi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz amethibitisha kumuua, Kamanda huyo aliyekuwa anasimamia mlango wa Bahari wa Hormuz, njia kuu ya meli za mafuta, iliyofungwa na Iran.

Israel imeongeza kuwa kuuawa kwa Kamanda huyo ni mfano wa ushirikiano dhabati kati ya majeshi ya nchi yake na Marekani.

Kuendelea kufungwa kwa Hormuz, kumeanza kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta katika mataifa mbalimbali, licha ya Iran kuendelea kukataa kuufungua mlango huo wa Bahari.

Wakati hayo yakijiri, Baraza la nchi za Ghuba limesema vitendo vya Iran kutekeleza mashambulio katika nchi jirani, vimevuka mistari yote nyekundu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *