Kaimu Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC ameonya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi kwamba mzozo mashariki mwa Kongo, eneo lenye utajiri wa madini unaongezeka na kuenea katika maeneo mengi, huku matumizi ya silaha nzito na ndege zisizo na rubani za kushambulia yakiongeza hatari kwa raia.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Vivian van de Perre amesema kwamba licha ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda na washirika wao kutoka mji wa Uvira chini ya shinikizo la kimataifa mwezi Januari, mapigano yanaongezeka katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini kati ya M23 na vikosi vya jeshi la Kongo na wafuasi wao.

Vivian van de Perre  amesema hali katika mkoa wa Kivu Kusini bado ni tete na kwamba kumezuka  uhasama mpya unaotanua mzozo huo  katika maeneo mengine ikiwa ni pamoja na mkoa wa Tshopo na eneo la mpakani mwa Burundi, hali ambayolinazidisha hatari ya kuzuka kwa vita vya kikanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *