
Jarida la Foreign Affairs la Marekani, limechunguza uwiano wa ushindi na hasara katika vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran na kuandika: Tehran inapata ushindi katika vita hivi.
Jarida hilo la Marekani limeeleza katika ripoti yenye kichwa cha maneno “Iran’s Long Game” kwamba Iran inatimiza malengo yake kutokana na matatizo ambayo imewasababishia maadui zake. Jarida hilo limeongeza kuwa maandalizi ya miongo kadhaa ya Iran yanazaa matunda.
Jarida la Foreign Affairs limeandika kwamba Iran kwa sasa inatekeleza mkakati ambao umeweza kuharibu mifumo kadhaa muhimu ya ulinzi wa anga ya Marekani na Israel, kuharibu vikali kambi za kijeshi za Marekani katika Ghuba ya Uajemi, kusababisha mashinikizo makubwa ya kiuchumi katika eneo hilo, na kuibua mgawanyiko kati ya Marekani na washirika wake wa Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi.
Kwa mujibu wa jarida hilo, Iran imesababisha matatizo makubwa ya kiuchumi na kisiasa kwa maadui zake, na pia inashikilia mpini katika ngazi ya kimkakati.
Jarida hilo la Marekani limesema kwamba vita vya sasa havipaswi kuhukumiwa kwa viwango vya kawaida, na kuongeza: “Kigezo sahihi cha tathmini si kama Iran inapigwa vibaya au la? Badala yake, swali litakalokuwa muhimu vita vitakapoisha ni kwamba Tehran itafikia malengo yake ya kimkakati au la? Kwa maana hii, Iran inashinda vita hivi.”