JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Gilbert Edwin Mwabulesi (26), mkazi wa Kijiji cha Ibililo, Wilaya ya Rungwe, kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi, Edwin Mwabulesi (65), kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, tukio hilo lilitokea Machi 21, 2026 majira ya saa 9:20 usiku katika Kitongoji cha Nsanga, Kijiji cha Ibililo, Kata ya Nkunga, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe.
Kamanda Kuzaga amesema mtuhumiwa alimshambulia baba yake kwa kumpiga ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili, hali iliyosababisha kifo chake.SOMA: Mpogolo: Wahusika mauaji ya mzee Salehe wakamatwe
