
MKUU wa Wilaya ya Tabora Upendo Wella, amepiga marufuku wakulima wa zao la korosho kuuza mazao yao nje ya mkoa huo, akiwataka kutumia mfumo wa stakabadhi ya ghala pamoja na minada ya kidijitali.
Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia changamoto za muda mrefu za masoko na gharama kubwa za usafirishaji ambazo zimekuwa zikiwakabili wakulima, hali iliyokuwa ikidhoofisha maendeleo ya zao hilo pamoja na kipato chao.

Amesema kuwa utekelezaji wa utaratibu huo utasaidia kupunguza gharama zisizo za lazima, kuongeza ushindani wa kibiashara, na kuhakikisha wakulima wanapata bei bora ya korosho zao.
Aidha, hatua hiyo inatarajiwa kuinua uchumi wa mkulima mmoja mmoja pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Tabora kwa ujumla. SOMA: Mauzo korosho yavuka tril 1.2/-