KIPAwa Young Africans SC, Djigui Diarra, amekumbana na adhabu ya kufungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya shilingi milioni nne kutokana na utovu wa nidhamu katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar FC uliopigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Taarifa iliyolewa leo jijini Dar-es-salaam na Tanzania Premier League Board imesema kuwa Diarra alipata adhabu ya michezo mitatu na faini ya shilingi milioni mbili kwa kumshambulia mwamuzi wa kati mara baada ya kumalizika kwa mchezo namba 126, uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Aidha, kipa huyo ametozwa faini nyingine ya shilingi milioni mbili kwa kuonesha ishara ya kidole cha kati alipokuwa akiondoka uwanjani kitendo kilichozingirwa kama matusi na dharau kinyume na kanuni za Ligi Kuu kuhusu nidhamu ya wachezaji. SOMA: Yanga inaongoza 1-0 ngoma mapumziko

Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri umeibua mjadala miongoni mwa wadau wa soka, huku tukio hilo likichukuliwa kama funzo kwa wachezaji wengine kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili na nidhamu ndani na nje ya uwanja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *