ARUSHA: Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Yusuph Singo, ameipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa maandalizi na mafanikio mazuri ya tukio la mbio za Arusha Night Jogging lililofanyika jijini Arusha.

Arusha night Jogging ilibeba kauli mbiu ya “Utamaduni wetu fahari yetu nufaika na Afcon 2027”

Maofisa mbalimbali wa utamaduni na Michezo, wilaya na mkoa, wananchi walishiriki mbio za kilometa 5 zilizohudhuriwapia na viongozi mbalimbali ambao kwa pamoja waliuungana katika kutoa hamasa ya michezo na mazoezi.

Akizungumza katika mbio hizo ambazo zimefanyika ikiwa ni moja ya maandalizi kuelekea kikao kazi cha 16 cha moafisa Utamaduni na Michezo, Singo aliwashukuru wote kwa ushirikiano wa kufanikisha tukio hilo na kusema ni katika kuendeleza juhudi hizo kukuza michezo ambayo pia ni afya.

“Naiomba Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo, kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa na maandalizi ya jogging kubwa zaidi itakayofanyika jijini Arusha na hii ni kutokana na mafanikio mazuri ya mbio,”alisema Singo.

Mgeni rasmi katika mbio hizo Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Boniface Tamba alitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa za kuhimiza maendeleo ya michezo nchini.

“AFCON ndio mpango mzima na tunaona mambo makubwa yanaendelea kwa serikali yetuinafanya maandalizi makubwa miundombinu ya viwanja vya michezo inayojengwa ikiwemo barabara ni uwekezaji mkubwa kwenye sekta zetu unaofanyika kwa ajili hiyo hivyo tumekuja hapa ili kuendelea kuchagiza na kila mmoja ajue,”alisema Tamba.

Aidha aliishukuru Wizara wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Waziri wake,Paul Makonda wanaohamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi pamoja na TAMISEMI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *