Huu ni uamuzi wa kihistiria wa Mahakama ya Utawala ya Paris siku ya Ijumaa, Machi 27. Zaidi ya miaka 80 baada ya mauaji ya Thiaroye, Mahakama ya Ufaransa imeihukumu Ufaransa  kwa kuficha mazingira ya mauaji haya yaliyofanywa na jeshi la kikoloni kwa askari wa Kiafrika, ambao walikuwa wakidai malipo yao ya nyuma baada ya kupigana katika safu ya jeshi la Ufaransa.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya utawala ya Ufaransa ilitambua hatia ya Ufaransa siku ya Ijumaa kwa kushindwa kutekeleza “hatua zinazoweza kutoa mwanga juu ya hali halisi” za kifo cha mmoja wa askari wa Kiafrika waliouawa na jeshi la Ufaransa mwaka wa 1944. Biram Senghor, mtoto wa askari wa Kiafrika aliyeuawa siku hiyo, ndiye aliyewasilisha kesi hiyo mahakamani.

Katika taarifa, Mahakama ya Utawala ya Paris ilibainisha kwamba “mamlaka ya Ufaransa,” baada ya “kutoa taarifa kadhaa zenye makosa” kwa familia ya mwanajeshi huyo katika miaka iliyofuata kifo chake, baadaye “ilishindwa kutekeleza njia zote zilizokuwa zinapatikana ili kutoa mwanga kuhusu mazingira sahihi ya kifo chake na mahali alipozikwa.”

Mnamo Desemba 1, 1944, jeshi lilifyatua risasi huko Thiaroye, karibu na Dakar, kwa askari hawa kutoka nchi kadhaa za Afrika Magharibi ambao walikuwa wakipigana kaika safu ya jeshi la Ufaransa na walikuwa wakidai malipo yao ya miezi ya nyuma ambayo walikuwa bado hawajalipwa. Mazingira ya mauaji hayo, idadi ya waliofariki, na mahali walipozikwa bado hayajafafanuliwa. Kiwewe cha mauaji haya kinashuhudiwa nchini Senegal na katika walikotoka askari wa Kiafrika waliopigana katika safu ya jeshi la Ufaransa: Mali (wakati huo ikiitwa Sudani ya Ufaransa, kulingana na jina lake la kikoloni), Côte d’Ivoire, Guinea, na Burkina Faso (zamani ikiitwa Upper Volta).

Mnamo mwezi Novemba 2024, usiku wa kuamkia miaka 80 ya matukio ya Desemba 1944, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikiri kwamba vikosi vya kikoloni vya Ufaransa vilifanya mauaji huko Thiaroye.

“Taarifa kadhaa potofu”

Bila kumtambua askari huyo, Mahakama ya Utawala ya Paris ilieleza kwamba haiwezi kuiwajibisha Ufaransa kwa kifo chenyewe, kutokana na sheria ya mipaka. “Kwa hivyo, inaweza tu kufidia uharibifu wa maadili unaohusiana na kushindwa kuchunguza mazingira sahihi ya kifo cha askari huyo” na hivyo kumpa mtoto wa askari huyo euro 10,000.

Mahakama ilibainisha kwamba “katika miaka iliyofuata kifo hicho,” Ufaransa ilitoa “taarifa kadhaa potofu kwa familia yake, ikisema kwamba alitoroka, kwamba malipo yake yalikuwa yamerejeshwa kikamilifu, na kwamba hatua ya askari wa Ufaransa kufyatua risasi ilikuwa jibu sawia kwa hali waliyokabiliana nayo.”

Ingawa baadaye walikiri kwamba ushuhuda huu “haukuhusiana na ukweli wa kihistoria,” wakikiri mnamo mwaka 2019 kwamba hakuwa mtoro na mnamo mwaka 2024 kwamba “alikufa kwa ajili ya Ufaransa,” mamlaka hata hivyo “ilishindwa kutekeleza njia zote zilizopatikana ili kutoa mwanga juu ya mazingira sahihi ya kifo chake na mahali alipozikwa.”

Kulingana na mahakama, “mapungufu katika kutekeleza njia zinazoweza kufafanua mazingira sahihi ya kifo chake lazima yachukuliwe kama kosa la aina ya kuwajibika kwa Serikali.”

“Kwa Biram Senghor, ni habari njema kujua kwamba Serikali imeamriwa kulipa kiasi fulani cha fidia. Hata hivyo, kinachonifanya niwe na uchungu kidogo ni kwamba hukumu kuhusu fidia ya mauaji ya baba yake si nzuri kabisa, ” amesema mwanahistoria Armelle Mabon, akibaini kwamba mapambano hayajaisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *