Ukraine imerusha zaidi ya ndege zisizo na rubani 430 kuelekea Moscow usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, ametangaza meya wa mji mkuu wa Urusi, Sergei Sobyanin, siku ambayo mkutano wa NATO unafunguliwa mjini Ankara huku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa mgeni wa heshima.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Kuanzia jioni hadi saa 12:00 asubuhi, zaidi ya ndege zisizo na rubani 430 ziliruka kuelekea eneo la Moscow. 

Nyingi ziliharibiwa na vikosi vya ulinzi wa anga kwa umbali mrefu. Ndege zisizo na rubani 36 za adui ziliharibiwa zilipokaribia Moscow,” Sobyanin ameandika kwenye mitandao ya kijamii. 

Wakati huo huo, “mashambulizi ya mara kwa mara” ya makombora ya Ukraine yalimuua angalau mtu mmoja na kuchoma miundombinu katika eneo la Belgorod nchini Urusi, ambalo linapakana na Ukraine, kulingana na kaimu gavana wa eneo hilo Alexander Shuvaev.

 Mashambulizi haya ya Ukraine yanakuja siku moja baada ya mashambulizi makali ya anga ya Urusi dhidi ya Ukraine, ambayo yamesababisha vifo vya angalau watu 28, wakiwemo 26 huko Kyiv, kulingana na mamlaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *