
Jaribio la shambulio kwa klipuzi limezimwa leo Jumamosi, Machi 28, jijini Paris, mbele ya tawi la Benki Kuu ya Amerika, Bank of America, baada ya maafisa wa polisi kuingilia kati na kumkamata mtu aliyekuwa akijiandaa kulipua kilipuzi hicho, shirika la habari la AFP limenukuu vyanzo vilivyo karibu na uchunguzi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ofisi ya mwendesha mashtaka dhidi ya ugaidi imetangaza kuwa kesi hiyo iko mikononi mwake na imeanza uchunguzi.
Tukio hilo lilitokea yapata saa 9:30 usiku wa kuamkia leo Jumamosi kwenye mtaa wa Boétie, magharibi-katikati mwa Paris, mbele ya jengo la Benk of Amerika. Maafisa wa polisi walimkamata mtu ambaye alikuwa ameweka kilipuzi hicho kilichotengenezwa kienyeji mbele ya jengo hilo. Kifaa hicho kilikuwa kinaundwa na dumu la lita 5 la kioevu, kinachowezekana kuwa hidrokaboni, na utaratibu wa kulipua, kulingana na moja ya vyanzo hivyo.
Uchunguzi umekabidhiwa kitengo kinachopambana na ugaidi kutoka kikosi cha uchunguzi wa jinai cha Paris.
“Hongera kwa uingiliaji kati wa haraka wa polisi wa mkoa ambao uliwezesha kuzuia kitendo cha kigaidijana usiku huko Paris,” ameandika Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurent Nuñez, kwenye mtandao wa kijamii wa X. “Uangalifu unaendelea kuliko hapo awali katika kiwango cha juu,” ameongeza.
Taarifa zaidi zinakujia…