Brighton huenda ikakubali kulegeza kamba katika msimamo wao kuhusu kiungo wao wa kimataifa wa Cameroon, Carlos Baleba, 22.

Awali Brighton ilikuwa ikihitaji ada ya Pauni 100 milioni na kuendelea ili kumuuza staa huyo lakini sasa ipo tayari kusikiliza ofa ambazo zitakuwa ni chini ya kiasi hicho cha pesa.

Hatua hiyo inatajwa kuwa huenda ikaufungua mlango kwa klabu mbalimbali kuingia kwenye mbio za kumsajili Baleba, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.

Kiungo wa kimataifa wa England, Adam Wharton. Picha na Mtandao

Adam Wharton

Kiungo wa kimataifa wa England, Adam Wharton, 22, anatajwa kuwa na mpango wa kuondoka Crystal Palace mwishoni mwa msimu huu.

Inaelezwa kuwa Manchester United, ambayo ni miongoni mwa klabu zinazomuwania, ina asilimia kubwa ya kumsajili kwani moja kati ya sharti ambalo aliwapa ni kuhakikisha wanafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya jambo ambalo linaonekana kuwa na zaidi ya asilimia 70 za kukamilika kutokana nafasi yao katika ligi. Wharton ni miongoni mwa viungo wenye kipaji kikubwa England.

Kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson. Picha na Mtandao

Elliot Anderson

Arsenal inaendelea kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson mwenye umri wa miaia 23, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hata hivyo, Arsenal haitakuwa peke yake katika mbio hizo, kwani Manchester City, Manchester United na Chelsea nazo ni miongoni mwa timu zinazotajwa kutaka kumsajili staa huyo.

Anderson ameonyesha kiwango bora sana akiwa na Forest kwa msimu huu licha ya timu yake kutokuwa na mwenendo mzuri katika ligi.

Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Aurelien Tchouameni. Picha na Mtandao

Aurelien Tchouameni

Manchester United na Liverpool zinamfuatilia kwa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Aurelien Tchouameni, 26, anayekipiga katika kikosi cha Real Madrid. Inaelezwa kuwa klabu zote mbili zinataka kuimarisha safu zao za kiungo, na Tchouaméni anaonekana kuwa chaguo bora kutokana na uwezo wake. Hata hivyo, Real Madrid haionekani kuwa na mpango wa kumuuza fundi huyo licha ya kutopata nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi chao cha kwanza.

Winga wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Georgia, Khvicha Kvaratskhelia. Picha na Mtandao

Khvicha Kvaratskhelia

Liverpool na Arsenal zimekumbana na pigo kubwa baada ya juhudi zao za kumsajili winga wa Paris Saint-Germain ma timu ya taifa ya Georgia, Khvicha Kvaratskhelia, 25, kukataliwa. Inaelezwa kuwa PSG haina mpango wa kumuachia nyota huyo, ambaye anaendelea kuwa sehemu muhimu ya kikosi chao, kutokana na kiwango chake.

Hatua hiyo inazilazimisha klabu hizo mbili kutafuta mbadala mwingine katika soko la usajili.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Ferran Torres. Picha na Mtandao

Ferran Torres

Manchester United imepewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Ferran Torres, 26, kutoka Barcelona katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Inaelezwa kuwa Barcelona iko tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya mchezaji huyo, jambo linaloweza kuwapa Man United nafasi ya kumsajili fundi huyo na kuimarisha safu yao ya ushambuliaji. Torres ambaye aliwahi kucheza Manchester City, kwa sasa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha Barca. Nyota huyo ameivutia sana Man United kwa sababu analifahamu vizuri soka la England.

Mshambuliaji Olympique de Marseille, Mason Greenwood. Picha na Mtandao

Mason Greenwood

Juventus imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji Olympique de Marseille, Mason Greenwood mwenye umri wa miaka 24, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hata hivyo, inatarajiwa kukutana na upinzani mkali kutoka kwa Atletico Madrid ambayo inaonekana kuwa mbele katika mbio hizo na imeshazungumza hadi na wawakilishi wa mchezaji. Hatma ya Greenwood katika kikosi cha Atletio bado haijajulikana ingawa inaaminika kwamba yeye mwenyewe pia anatamani kuondoka

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *