
Katika hotuba ya televisheni kwa taifa, rais wa Marekani amepongeza ushindi “wa maamuzi” na “wa kushangaza” dhidi ya Iran tangu kuanza kwa operesheni za pamoja za Israel na Marekani mnamo Februari 28.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Marekani amedai kwamba Marekani “iko karibu kufikia” malengo yake ya kimkakati nchini Iran, hasa kwa kuzuia Tehran kupata silaha ya nyuklia.
Wakati wa hotuba yake kwa taifa, Rais Trump alisema kwamba Iran “si tishio tena.”
“Iran imeangamizwa, na sehemu ngumu zaidi imekwisha,” alisema.
Donald Trump aliahidi Jumatano kuishambulia Iran bila kuchoka kwa wiki nyingine mbili hadi tatu, akitishia mitambo yake ya umeme haswa.
“Tutawashambulia vikali sana katika wiki mbili hadi tatu zijazo. Tutawarudisha kwenye Enzi ya Mawe, ambapo ndio sehemu yao.” “Wakati huo huo, majadiliano yanaendelea,” rais wa Marekani amesema katika hotuba kwa kwa taifa kutoka Ikulu ya White House.
“Ikiwa hakuna makubaliano, tutapiga kila moja ya mitambo yao ya umeme kwa nguvu sana na pengine kwa wakati mmoja,” ameongeza.