MAPIGANO kati ya Iran na Israel yameendelea huku pande hizo zikishambuliana kwa makombora na droni. Hatua hiyo inakuja wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kupiga kura kuhusu usalama wa mlango-bahari wa Hormuz.

Iran imesema bado ina uwezo mkubwa wa kijeshi licha ya kauli ya Donald Trump kuwa umeathirika. Israel imedai kumuua kamanda wa Iran, Jamshid Eshaghi, katika shambulio la Tehran. Nchini Lebanon, watu 27 wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi dhidi ya makundi yanayoungwa mkono na Iran.

Pia, mashambulizi ya anga ndani ya Iran yamelenga miundombinu muhimu na kusababisha vifo na majeruhi. Iran imekosoa mashambulizi hayo ikisema hayatailazimisha kusalimu amri. Wakati huo huo, waasi wa Kihouthi nchini Yemen wamesema wamerusha makombora kuelekea Israel kwa kushirikiana na Iran na Hezbollah. SOMA: Iran yaikosoa Israel kuhusu usitishaji mapigano

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *